Harmonize – Vibaya Lyrics

Harmonize Vibaya LyricsVibaya Lyrics Harmonize

B Boy mmmh
Oa aaah, oooh aaah
Oooh aah…ooooh

Alisema mapenzi vita
Mi na yeye tuungane kuwateketeza maadui
Eeh maadui
Badala ya miezi kupita aah
Vikombe lazima vigongane
Na sio kwamba hayajui, eeh hayajui

Pigo za kusema vya ndani mi sinaga hizo
Ama kumtafuta mchawi ni nani ni kuongeza tatizo
Tulia hapa tutakuwa wa ndani hadi paradiso
Na tukatangaza kweupe mambo ya hadharani
Na tattoo ndo hizo, oh oh ohhh

Sitaki kuamini kwamba
Lile kapu la mabaya yangu
Halina hata machache mema oh mema
Nitakuwa mshamba
Nikiyasema yote mabaya ya mwenzangu
Ili nionekane mwema

Japo mapenzi yanaumiza
I wish tusisemane (Vibaya vibaya)
Ili kesho tusizikane (Vibaya vibaya)
Usiwasikilize wapambe (Vibaya vibaya)
Wanachotaka maneno ili kesho watuchambe (Vibaya vibaya)

Oa aaah, oooh aaah
Oooh aah…ooooh mmmh

Nitunzie siri zangu
Nami nitunze zako za miaka rudi nenda
Kuna leo na kesho mmh mmh mmh
Hata maadui zangu walikuwaga maadui zako
Hawawezi kukupenda wanakuvuta uwe kichekesho

Mmmh mmh mmh
Maana hata ukisambaza
Picha zangu za aibu ni sawa, hata hunikomoi
Na hata utupu wako ukiutandaza
Kwa watu wangu wa karibu sio doa, hujengi hubomoi

Mama kuna kamchezo mtunze mtoto wako
Na watu wenye majungu (Majungu)
Nilikubali kuviacha vya dezo
Sababu ya mapenzi yako nikaachana na mzungu (Mzungu)

Maneno yao utadhani wanakutetea
Kumbe tudhalilishane wanachongojea
Usiwape faida wambea
Na ni kama kawaida nakuombea

Sitaki kuamini kwamba
Lile kapu la mabaya yangu
Halina hata machache mema oh mema
Nitakuwa mshamba
Nikiyasema yote mabaya ya mwenzangu
Ili nionekane mwema

Japo mapenzi yanaumiza
I wish tusisemane (Vibaya vibaya)
Ili kesho tusizikane (Vibaya vibaya)
Usiwasikilize wapambe (Vibaya vibaya)
Wanachotaka maneno ili kesho watuchambe (Vibaya vibaya)

Oa aaah, oooh aaah
Oooh aah, ooh aah…ooooh mmmh

(Konde Music Worldwide)
B Boy thank you for the sound
Sound…Sound

Written by; Harmonize

Harmonize Vibaya Lyrics